|
|||
|
Kundi la Xplastaz linawakilishwa na wasanii watatu, NELSON CHRIZOSTOM RUTTA a.k.a. FAZA a.k.a. RUFNELLY, ABDALAH FAROUK MINJA aka ZIGGY-LAH na GODSON CHRIZOSTOM RUTTA a.k.a. GSON. Pia kuna Mmasai, huyu huupamba music wao kwa kuweka vionjo vya asili ya Kimasai. Alijiunga na kundi hili baada ya kuonekana kuwa mahiri sana katika kuimba nyimbo za Kimasai huko kijijini kwao MONDULI JUU, yeye anaitwa YAMAT OLE MEIPUKO a.k.a. MEREGE (gonga hapa kwa kusoma zaidi kuhusu Merege!). Mwingine ni SIMON BINARA yeye alijiunga na kundi hili muda mfupi kabla ya kwenda Ubelgiji ambapo anaendelea na shughuli za kimuziki. Mahali walipozaliwa na kukulia Wote walizaliwa mjini Arusha. Faza aka Ruffnelly alizaliwa mwaka 1976 katika hospitali ya mount Meru, na alikulia Arusha na kusomea ktk shule ya msingi Kijenge, baada ya kumaliza elimu yake ya msingi alipata nafasi ya kwendelea na masomo ya katika shule ya secondary, Arusha secondary school iliyopo mjini Arusha na kumaliza masomo yake mwaka 1996. Hakupata nafasi ya kuweza kuendelea na masomo ya kidato cha 5 na kuendelea kufanya kazi ndogondogo pamoja na hii fani ya music wa rap. Gson ni ndugu yake na Ruf. Yeye pia alisoma shule ya msingi Kijenge na kuendelea na kidato cha kwanza Arusha secondary school ya mjini Arusha. Alipomaliza kidato cha nne aliendelea na kazi za usanii na utafiti wa asili ya vitu mbalimbali vya Kiafrica hasa Kimasai na kazi za kitalii. Ziggy alizaliwa mjini Arusha na baadae alisoma shule ya msingi Manyara Range ya huko Manyara Arusha. Alipomaliza alikwenda kumalizia masomo yake katika shule ya secondary ya Minja mkoani Kilimanjaro. Hakupata nafasi ya kuendelea na alikwenda mjini Dar-es-salaam na baadae Tanga na mnamo mwaka 1993 alirudi Arusha mjini ndipo alipokutana na wenzake Gson na Nelly. Kilichopelekea kuanza music Kabla ya kuwa wanamuziki ktk hii fani ya hiphop , tulikuwa tukipenda sana muziki kila aina kwani tulishawahi kuwa underground dancers wa miziki iliyokuwa ikipendwa na jamii. Tulitokea kuupenda sana music wa hiphop kutokana na hisia, mizuka na ujumbe mzito unaoweza kuifikia jamii kwa urahisi. Hii ilikuwa ni baada ya rap kuanza kuutingisha ulimwengu wa muziki na kutokea kupendwa na vijana wengi baada ya kuingia hapa nchini. Tulipenda kusikiliza nyimbo za crew mbalimbali kutoka Marekani kama Mc Hammer, NWA, Leaders of the new school, Cold Crush, Wu Tang, Lords of the underground, Onyx, Naughty by Nature nk. Baadaye tulianza kusikia nyimbo za Saleh Jabir, alizozibadilisha kutoka katika Kingereza kwenda katika Kiswahili na baadae tuliwasikia wasanii wengine kama Mr 2 nk. Hapo ndipo tulipopata hisia na gadhabu ya kuanza kutunga na kuandika nyimbo zetu ktk Kiswahili. Tulianza kuperform ktk kumbi mbalimbali za starehe kama CAVE DISCO, BY NIGHT DISCO, METROPOLE DISCO na CHIK KING a.i.c.c. mjini Arusha, pamoja na katika kumbi za starehe. Kuanzishwa kwa kundi Kabla ya kuanza kundi hili, kila mmoja wetu alikuwa msanii wa kujitegemea (solo artist). Tulikuwa tukifahamiana kutokana na kukutana kila mara katika kumbi za disco, maonyesho na sehemu mbalimbali na zilizokuwa zikikutanisha vijana waliokuwa wakiupenda muziki huu wa rap. Baadae Ziggy aliyekuwa akijulikana kama Dr Abby alikwenda mjini Dar-es Salaam akiendelea na masomo. Wakati huo Ruf aliyekuwa maarufu kwa jina la R’nell alikuwa akiendelea na masomo yake mjini Arusha na Gson. Mwaka 1993 baadae Rufnelly na Ziggy tulikutana tena ndipo tulipoanzisha kundi lililokuwa likijulikana kwa la 2 Rough G’z na siku hiyohiyo tulifanikiwa kuandika wimbo wa Bamiza uliopelekea sisi kujulikana katika anga za music hapa Tanzania na nje ya nchi. Mwaka 1996 tuliamua kubadili jina na kujiita Xplastaz baada ya kugundua kuwa jina lile halitakuwa kivutio zaidi katika jamii ya baadae. Mwaka huo huo tulikutana na mwandishi wa habari Peter kutoka Uholanzi alipofika mjini Arusha kufanya utafiti na uhamasishaji wa muziki wa rap, akiwa na Mr 2, Diplomatz na 4 crewz flava toka mjini Dar. Tulijumuika pamoja na wasanii wengine katika ukumbi wa Mawingu Club na kufanya onyesho kwa ushirikiano na upendo, tukiwa kama wenyeji wao. Promota alikubali kazi na baada ya shoo, tuliongea naye na baada ya mahojiano, tulimwachia address zetu na kutuahidi kufikisha ujumbe ule kwa rafiki yake aitwaye Thomas Gesthuizen ambaye alitutumia barua ya kwanza miezi michache baadaye. Tuliendelea kuwasiliana mpaka mwaka 1997, Thomas alipokuja hapa nchini na kufanikiwa kufika mjini Arusha na kurecord wimbo wetu wa kwanza uitwao Bamiza, akishirikiana na Dj Muddy-G wa Arusha. Wimbo huu ndiyo uliotupatia jina na umaarufu katika anga za muziki na kututangaza ndani na nje ya nchi na kupigwa katika kumbi mbalimbali za disco na starehe. Mwaka 1998 tulirecord wimbo mwingine unaojulikana kama Wacha piga chata. Mwaka 1999 tulifanya tulipata bahati ya kuwepo katika documentary iliyofanywa kwa ushirikiano wa wasanii mbalimbali wa hapa nchini, chini ya usimamizi wa Martin a.k.a Mongo star na uongozi mzima wa kampuni ya MADUNIA kutoka Uholanzi. Hii nayo ilisaidia kututangaza nje na ndani ya nchi. Mwaka 2000 tulishoot video ya wimbo Bamiza, iliyofanyiwa matayarisho huko nchini Uholanzi chini ya usimamizi wa Thomas. Video hii ilitokea kuwa kivutio na gumzo kwa walioiona kupitia radio station mbalimbali za hapa nchini na nje ya nchi. Mafanikio Kutokana na uvumilivu, ushirikiano na mawasiliano ya karibu na wadhamini wetu na watu mbalimbali wa hapa nchini na nje ya nchi, mwanzoni mwa mwaka 2001 tulipata kujumuika na wasanii wengine kutoka nchi za Uholanzi na Africa ya kusini EJ, Devious, 2Tall na Skate the Great pamoja na wasanii wengine toka hapa nchini. Tulifanya semina mbalimbali katika ukumbi wa Simba Grill - Kilimanjaro hotel, na shoo iliyofanyika katika ukumbi wa FM club na baadaye tulirecord track mbili ‘Round table' na 'Life in a day', zilizowashirikisha pia wasanii wadogo Fortune Tellers toka Arusha na Hashim a.k.a Dogo na wengineo, chini ya maproducer Pfank, Master J wa hapa nchini na 2Tall wa Uholanzi. Tumepata bahati ya kurecord albam nzima yenye nyimbo 13 inayokwenda kwa jina la Ushanta iliyomalizikia kutengenezwa nchini Uholanzi, chini ya utayarishaji wa maproducers Halfan a.k.a Pfunk na Raymond a.k.a. Kid Sundance chini ya udhamini wa kampuni ya Madunia iliyopo Uholanzi. Tumefanikiwa pia kutengeneza video nyingine ya wimbo huo, Ushanta chini ya usimamizi wa Thomas Gesthauzin a.k.a Juma4. Tulipata mwaliko wa kwenda nchi za Uhollanzi na Ubelgiji kufanya maonyesho na Festival Mundial katika miji mbalimbali ya nchi hizo na kufanikiwa kujitangaza Ulaya pamoja na kuitangaza nchi yetu katika sekta mbalimbali kama vile kiutamaduni, utalii, uwekezaji na hiphop ya Kiswahili. Baadhi ya wageni wameshakuja nchini na wengine wanatarajia kuja kwa ajili ya kuhamasisha na kuinua kiwango cha muziki wa hiphop. Tulichojifunza kutokana na safari ya uholanzi Ubelgiji, Uholanzi na Ulaya nzima, ni tofauti sana na nchi yetu ya Tanzania kimaendeleo, kiuchumi na mambo mengine mengi sana. Tumepata kukutana Mc’s na watu wa aina nyingine tofauti, maisha, hali ya hewa na masaa vinatofautiana sana. Tulichojifunza zaidi ni kuona wasanii wa kule wanavyokuwa na ushirikiano mkubwa kikazi, mikutano na vikao vya kila mara, kuongelea matatizo yanayowakabili, kutetea haki zao kwa nguvu na kupeleka malalamiko yao kwa vyombo husika na kusaidiwa. Umoja wao umefanya wasanii wathaminiwe na kufanya muziki kuwa kazi inayowaendeshea maisha yao ya kila siku, kufaidika kutokana na musiki. Uzoefu wa kuandaa shoo na kuperform mbele ya umati wa watu wengi zaidi ya 100,000 pamoja na uzoefu wa kuongea na waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari. Pia tumefanikiwa kuitangaza nchi yetu katika sekta mbalimbali kama vile kiutalii, kisiasa, uwekezaji kidini. Mipango Kwa sasa tunamalizia mambo ya mikataba na makubaliano mbali mbali na hivi karibuni tunategemea kutoa na kuzindua cd-single na albam yetu yenye nyimbo 13 itakayokuwa katika soko hivi karibuni. Albam hiyo inakwenda kwa jina la Ushanta, pia video na website yetu ijulikanayo kama www.xplastaz.com. Pia tuna mpango wa kutoa video na wimbo wa Ushanta utakaosikika na kuonekana katika radio na tv station mbalimbali hivi karibuni. Albam hiyo inashirikisha baadhi ya wasanii wa hapa Tz kama Hashim a.k.a Dogo, Fortune tellers nk. Ujumbe tunaotoa ktk nyimbo zetu Kadri siku zinavyozidi kwenda na watanzania wanazidi kuelimika kupitia muziki wa hiphop na jamii nzima imeonekana kuupokea vizuri kutokana na kusikiliza sana Bongo flava. Nyimbo zetu zinagusa sana hisia za wasikilizaji kwani zina ujumbe mzito unaoongelea mambo yanayoizunguka jamii mfano; siasa, dini, vita, familia, elimu na utamaduni na dunia nzima bjinsi inavyokwenda. Matatizo Tukiwa kama wasanii na kioo cha jamii, tunapata matatizo mengi, mfano matatizo ya fedha za kuingilia studio, na mahitaji muhimu kutokana na wasanii wengi kutoka katika familia duni au kuonekana wahuni katika jamii na kutengwa na familia zao kwa kuonekana-kana kwamba ni wahuni katika jamii. Serikali haipendi kuwa karibu na wasanii na kutotujali. Swala lingine linalotutatiza sisi wasanii wa Kitanzania ni hati miliki. Serikali imekuwa ikilipuuzia na kulifumbia macho jambo la Copyrights na sheria hii kuonekana haifanyi kazi ipasavyo. Kwani tunadhulumiwa sana katika uuzaji wa kazi zetu na katika matamasha na maonyesho mbalimbali tunayoyafanya. Matatizo ya kisanii Wasanii wa Tanzania hatuna Umoja, ushirikiano, upendo na Umoja. Hili jambo nalo linachangia kuwa vipaji vya wasanii wanaochipukia. Wasanii kupigana majungu live na kufanya muziki huu kudharaulika na watu wa rika na tabaka Fulani. Hii imewafanya baadhi ya wasanii kuandika na kuimba nyimbo zisizo na ujumbe katika jamii. Pia imepelekea wasanii kujenga chuki baina ya wasanii na maproducer, kutokana na baadhi ya wasanii kuongea lugha chafu na uchochezi, chuki, ugomvi na kujenga tabaka la ma mc Fulani linalotaka kuvuruga maendelea ya hiphop hapa nchini. Maproducers kuwa na ahadi za uongo, maringo na kinyongo kwa baadhi ya wasanii na wakati mwingine kupelekea baadhi ya radio kubagua kazi za wasanii wengine. Kuleta ugomvi katika sehemu za starehe na kumbi mbalimbali za disco na maonyesho ya hiphop baina ya wasanii kwa wasanii na mashabiki. Matarajio Mtarajio ni kuendeleza fani yetu ya sanaa ya muziki kwa sababu inaonyesha mafanikio. Tunapenda kufanikiwa zaidi kimuziki na kusoma zaidi ili baadae tuweze kuwa maproducer wazuri tuweze kuwasaidia wengine wanaochipukia na kusaidia familia zetu ili jamii ikubali kuwa muziki ni kazi. Kila mmoja wetu katika crew ya Xplastaz ana matarajio ya kurecord albam yake pekee. Ujumbe Fani ya muziki ni kazi kama kazi nyingine na wala siyo uhuni kama wazazi wengine wanavyodhani kuwa wanamuziki wa hiphop ni wahuni sana na wabakaji, wezi, walevi. Maoni Hiphop siyo wizi wala si kushindwa maisha, hiphop huelimisha, huburudisha na kuchochea mabadiliko kwani ujira mgumu. Tupende miziki yetu kwani hata nje utapendwa, Tusidharau kazi za wengine, Tuwe na ushirikiano mzuri kwani ndiyo utakaoleta maendeleo katika ulimwengu wa muziki kwani sisi wasanii ni kioo cha jamii kila mtu anajiangalia. Shukurani Shukurani zetu nyingi ziende kwa wale wenye moyo wa kuendeleza fani hii ya hiphop kama vile’ vyombo vya habari kama Radio, TV station, magazeti, mtandao na Ma DJ na watangazaji mfano Sebastian Maganga & Benard Oduor (Maasai promotions), wasambazaji wa muziki hapa nchini mfano; Mamu stores, FK Mitta n.k. Shukurani nyingine za pekee ziuendee uongozi mzima wa Madunia na festival mundial, wazazi waliotuunga nkono na mashabiki wa hapa nchini na nje ya nchi. Mwisho ni kwa ma producers, Pfunk, Mika Mwamba, Ludigo, Master J, DJ Muddy Guy na Raymond a.k.a Sundance. |